Kibalaesang

Kibalaesang (pia Kipajo) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabalaesang kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kibalaesang imehesabiwa kuwa watu 3200. Kwa vile Wabalaesang wengi wameanza kuacha lugha yao, Kibalaesang imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibalaesang iko katika kundi la Kicelebiki.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search